Serengeti Boys ya 2019 yaandaliwa

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) linaanza kuwafanyia majaribio vijana 39 walio chini ya miaka 15 kwa lengo la kuunda timu ya vijana itakayocheza fainali za Afrika mwaka 2019.

Ofisa Habari wa TFF, Alfred Lucas amesema kuwa vijana hao walikusanywa kutoka mikoa mbalimbali ya Tanzania.

"Hawa vijana watakuwa hapa kwa wiki moja na watachujwa na kubaki  wachezaji wachache watakaoungana na wachezaji waliopo Mwanza kuunda timu ya taifa," amesema Lucas.

Tanzania itakuwa mwenyeji wa fainali za vijana Afrika zitakazofanyika mwaka 2019.