Serengeti Boys kupokewa leo mchana JNIA

Muktasari:

Serengeti Boys inatarajiwa kutua Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam,  kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini ikitokea Libreville, Gabon kupitia Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Dar es Salaam. Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dk Harrison Mwakyembe ataongoza viongozi na wanafamilia wengine wa michezo hususani mpira wa miguu kuilakini Serengeti Boys katika Uwanja wa  Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) leo Jumatano saa 8:50 mchana.

Serengeti Boys inatarajiwa kutua Uwanja wa Kimataifa wa Ndege wa Julius Nyerere, Dar es Salaam,  kwa ndege ya Shirika la Ndege la Afrika Kusini ikitokea Libreville, Gabon kupitia Johannesburg nchini Afrika Kusini.

Mara baada ya kutua, timu itakwenda Hoteli ya Urban Rose kupata mapumziko ya siku moja kabla ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) kuandaa utaratibu wa kuagana nao.

Rais wa TFF, Jamal Malinzi alisema wanashukuru kwa uamuzi wa waziri kuungana na familia ya wanamichezo kuilaki timu hiyo.

“Timu hii sasa itabadilishwa na kuwa timu ya vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes,” alisema Malinzi.

Serengeti Boys iliyokuwa Kundi B iliondolewa Kundi B iliondolewa na Niger iliyopenya kwenda hatua ya nusu fainali kwa faida ya kupata ushindi katika mchezo ambao umekutanisha timu hizo kwani Tanzania ilifungwa 1-0 katika mchezo wa mwisho hatua ya makundi.  

 

Endelea kufuatilia mtandao wetu ili kupata taarifa za mara kwa mara kuhusu ujio wa Serengeti Boys.