Sane ambipu Kocha Guardiola

Wednesday April 19 2017

 

By London, England.

Kiungo wa Manchester City, Leroy Sane amemshukuru Kocha wake, Pep Guardiola kutokana na kumsaidia kwenye mazoezi na kuimarika.

Hata hivyo, mchezaji huyo na kocha wake, iliripotiwa kutokuwa na maelewano hivi karibuni wakati Man City ilipofunga mabao 3-0 dhidi ya Southampton mchezo uliopigwa kwenye Uwanja wa St Mary Jumapili iliyopita.

Mjerumani huyo aliyesajiliwa  Etihad akitokea Schalke 04 msimu uliopita kwa dau la Pauni 32 milioni  pamoja na marupurupu mengine kulingana na kiwango chake uwanjani takribani anapokea Pauni 11  milioni.

Tangu ametua hapo amefunga mabao tisa akisaidia kutoa pasi tatu zilizozaa mabao na amecheza mechi 30 za ligi msimu huu.

Juhudi za kocha Guardiola kwa mchezaji huyo zimemrejesha katika kiwango chake, hivyo kuwamo katika majina yaliyopendekezwa kuwania Tuzo ya Mchezaji bora wa Ligi Kuu England.

ìAlinifanya niwe miongoni mwa wachezaji mahiri wa kati licha ya kwamba nimekuwa nikicheza nafasi mbalimbali.

 ìNimekuwa mchezaji wa kutegemewa na ninamiliki mpira vyema.

Awali ililipotiwa kuwa, kocha huyo Mhispania, alitaka mchezaji huyo apiwe penalti baada ya kuchezewa faulo na Fraser Forster, lakini Sane alipingana na alichokuwa anakipigania kocha wake. Hivyo  refa aliamuru iwe kona.

ìNinachomshangaa hakutumia mbinu za kimchezo, kanuni ni kanuni tu, iwapo Sane alisema hivyo basi inabidi nimuamini,î alisema Guardiola.