Samatta haina kufelii kabisa

NYOTA wa Kimataifa wa Tanzania, Mbwana Samatta amewapa makavu nyota wa Ligi Kuu Bara kwa kuwataka wapambane mpaka tone la mwisho kuhakikisha wanatoka kwenda kucheza soka la kulipwa nje ya nchi.

Samatta ambaye amewahi kushinda tuzo ya Mchezaji Bora wa Afrika 2015, alisema mchezaji akipata nafasi ya kwenda kufanya majaribio asikubali tena kurudi Bongo mpaka mbinu zote zifeli.

“Nilianza kuwaelekeza wachezaji wenzangu juu ya faida ya kucheza soka nje na mmoja wa wachezaji ambao nilikuwa nawaelekeza kila siku ni Farid Mussa na nashukuiru sana kwa kunisikiliza na kulitimiza lile ambalo nilikuwa nikimwelekeza,” alisema Samatta.

“Mchezaji anapopata nafasi ya kwenda kucheza nje asikubali kufeli kirahisi. Nafasi hizo ni chache. Ikitokea ameshindwa arudi kujipanga upya na kutoka tena,” alisisitiza.

Kwa upande mwingine, Samatta alisema ipo haja ya kutafutwa kwa wachezaji wa kariba ya Thomas Ulimwengu katika timu ya taifa kwani kukosekana kwake kumekuwa pigo kubwa.