Samata aing’arisha Genk ugenini

Mbwana Samata

Muktasari:

Ushindi huo umeifanya Genk kufikisha ponti 31 na kusalia katika nafasi ya nane kwenye ligi hiyo yenye timu 16 pekee.

Bao pekee lililofungwa na Mtanzania Mbwana Samata katika dakika ya 82 laipa Genk ushindi wa 1-0 dhidi ya Eupen katika mechi ya Ligi Kuu Ubelgiji

Ushindi huo umeifanya Genk kufikisha ponti 31 na kusalia katika nafasi ya nane kwenye ligi hiyo yenye timu 16 pekee.

Genk inafungana pointi na Standard Liege ambayo katika msimamo wa ligi hiyo, ipo katika nafasi ya tisa. 

Club Brugge ni vinara wa ligi hiyo wakiwa na pointi 43, wakifuatiwa na Zulte-Waregem huku Anderlecht ikiwa nafasi ya tatu ikiwa imejikusanyia pointi 41.

Timu tatu zinazoburuza mkia katika ligi hiyo ni Waasland-Beveren, Royal Excel Mouscron na Westerlo.