Rufaa za timu zalitesha Shirikisho la Soka Ufaransa

Muktasari:

Mechi hiyo inayolalamikiwa, iliahirishwa kutokana na vurugu zilizotokea dakika ya 55 wa mchezo timu hizo zikiwa hazijafungana.

Shirikisho la Soka Ufaransa (FFF) limetupilia mbali rufaa ya Bastia kupinga uamuzi wa kuipa ushindi Lyon katika mechi iliyochezwa mwezi Aprili.

Mechi hiyo inayolalamikiwa, iliahirishwa kutokana na vurugu zilizotokea dakika ya 55 wa mchezo timu hizo zikiwa hazijafungana.

Wachezaji wa Bastia wanadaiwa kuingia uwanjani na kuwafanyia vurugu wachezaji wa Lyon kutokana na kutoridhishwa adhabu iliyokuwa imetolewa na mwamuzi.