Real yataja dau la kufuru kwa Mbappe

Muktasari:

Mshambuliaji huyo wa Monaco mwenye miaka 18, amezivutia klabu nyingi kubwa Ulaya baada ya kuonyesha kiwango cha katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa kuanzia hatua ya mtoano.
Mbappe amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mechi zote za hatua ya mtoano nyumbani na ugenini dhidi ya Manchester City na Borussia Dortmund.

Rais wa Real Madrid, Florentino Perez yupo tayari kutumia pauni 85milioni ili kumsajili mshambuliaji chipukizi Kylian Mbappe ikiwa ni moja ya sera yaka kuelekea uchaguzi ujao wa miamba hiyo ya Hispania. Gazeti la Ufaransa la LíEquipe limeripoti kuwaPerez amesema yupo tayari kufanya kila kitu kuhakikisha chipukizi huyo Mfaransa anatua Bernabeu na amejiandaa kutumia pauni 85milioni kwa ajili yake.
Mshambuliaji huyo wa Monaco mwenye miaka 18, amezivutia klabu nyingi kubwa Ulaya baada ya kuonyesha kiwango cha katika mashindano ya Ligi ya Mabingwa kuanzia hatua ya mtoano.
Mbappe amekuwa mchezaji wa kwanza kufunga mechi zote za hatua ya mtoano nyumbani na ugenini dhidi ya Manchester City na Borussia Dortmund.
Manchester United na Barcelona ni miongoni mwa klabu zinazohusisha kumtaka mshambuliaji huyo.