Real yapewa Atletico, Juve kwa Monaco Nyon, Uswisi

Muktasari:

Mechi ya Real na Atletico ni marudio ya fainali ya msimu uliopita, mahasimu hao wa jiji la Madrid watakutana katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Bernabeu hapo Mei  na marudiano wiki moja baadaye kwenye Uwanja wa Vicente Calderon kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana jiji Nyon, Uswisi.

Real Madrid na Atletico Madrid zitakutana katika nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa huku Juventus ikionyeshana kazi na Monaco.

Mechi ya Real na Atletico ni marudio ya fainali ya msimu uliopita, mahasimu hao wa jiji la Madrid watakutana katika mechi ya kwanza kwenye Uwanja wa Bernabeu hapo Mei  na marudiano wiki moja baadaye kwenye Uwanja wa Vicente Calderon kwa mujibu wa ratiba iliyopangwa jana jiji Nyon, Uswisi.

Monaco itakuwa wenyeji wa mabingwa wa Serie A, Juventus kwenye Uwanja wa Stade Louis II hapo Mei 3 kabla ya kusafiri kwenda Turin kwa mechi ya marudiano Mei 10.

Fainali ya mashindano hayo itafanyika Juni 3, kwenye Uwanja wa Cardiff's Principality, hii ni mara ya kwanza kwa fainali ya Ligi ya Mabingwa kufanyika nchini Wales.