Real Madrid yapania kuiteka Barcelona El Clasico

Wednesday April 19 2017

 

By Madrid, Hispania.

Kiungo Luka Modric amewasifu mashabiki wa Real Madrid kwa kujitokeza kwa wingi kuishudia timu yao ikishinda dhidi ya Bayern Munich na sasa anawataka wafanye hivyo katika mechi ya El Clasico dhidi ya Barcelona Jumapili hii.

Mabingwa hao watetezi wa Ligi ya Mabingwa, walisonga mbele baada ya kuifunga Bayern Munich  kwa jumla ya mabao 6-3 baada ya kumalizika mechi hiyo kwa ushindi wa mabao 4-2.

Mshambuliaji Cristiano Ronaldo alifunga ëhat trickí yake ya kwanza katika mashindano hayo na kiungo Arturo Vidal alitolewa nje kwa kadi nyeundu ya uamuzi wa utata kutoka kwa mwamuzi wa mchezo huo.

Hata hivyo, Modric alielekeza maoni yake kwenye mchezo wa Jumapili kati ya Barcelona na Madrid utakaoamua hatima ya ubingwa wa La Liga.

ìTulicheza kwa kiwango kikubwa na tumekuwa timu ya kwanza kutinga nusu fainali,î alisema Modric.

ìTunafuraha kuingia nusu fainali na sasa kilichobaki ni kushinda michezo inayokuja ili tuwe na uhakika wa kutetea ubingwa  kwa mara ya kwanza katika historia ya mashindano haya.

ìTunakabiliwa na mchezo mwingine mgumu Jumapili, tukishinda mchezo huo tutakuwa tumejitengenezea njia ya kutwaa ubingwa wa La Liga msimu huu.

ìTunahitaji kupata mapumziko kama kweli tunahitaji kucheza vyema katika mchezo unaokuja inabidi tupambane kama tulivyofanya kwenye mechi ya Bayern Munich,î alisema Modric.