Rais wa zamani Barcelona adakwa na polisi, mali zake zataifishwa

Muktasari:

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa El Confidencial imeeleza watu wengine nane wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa nyumbani na ofisini kaskazini mwa Catalonia.

Barcelona, Hispania. Rais wa zamani wa Barcelona, Sandro Rosell amekamatwa  kutokana nakosa la utakatishaji fedha.

Taarifa iliyotolewa na mtandao wa El Confidencial imeeleza watu wengine nane wanashikiliwa na polisi baada ya kukamatwa nyumbani na ofisini kaskazini mwa Catalonia.

Rosell alikuwa Rais wa Barcelona mwaka 2010 hadi 2014 na alijiuzulu wakati mahakama ilipoamuru uchunguzi ufanyike dhidi yake mwaka 2013 baada ya kuwapo na tuhuma za upigwaji fedha wakati wa mkataba wa kumsajili mchezaji wa kimataifa wa Brazil, Neymar.

Klabu ililipa Pauni 5.5 mwezi Juni 2016 kuhusiana na uhamisho wa Neymar akitokea antos ambaye naye alijumuishwa kwenye ukwepaji kodi.

Pia mke wa Rosell amekamatwa leo Jumannehuku El Confidencila ukieleza kwamba watuhumiwa hao ni sehemu muhimu kwa uchunguzi wa Hispania na FBI ambao wanafuatilia suala la rushwa jinsi fedha zilivyopenyezwa kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa).

Jaji wa mahaman, Carmen Lamela ameamuru kuziwa fedha zote zilizokuwa benki Pauni 10 milioni na mali nyingine zenye thamani ya Pauni 25 milion ambazo zilikuwa zinamilikiwa na rais huyo wa zamani.