Rais wa Fifa, Infantino aipongeza Yanga

Muktasari:

Rais, Infantino alituma ujumbe wake Mei 24, wa kuipongeza Yanga kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.

Dar es Salaam.Rais wa Shirikisho la Soka Duniani (Fifa), Gianni Infantino ameipongeza Yanga kwa kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.

Rais, Infantino alituma ujumbe wake Mei 24, wa kuipongeza Yanga kupitia Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)  kwa kutwaa ubingwa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara msimu wa 2016/17.

Yanga imetwaa kombe hilo kwa mara tatu mfululizo na katika salamu za pongezi, Rais Infantino amesema ubingwa huo wa Yanga ni kielelezo cha ushirikiano baina ya wachezaji, kocha, utawala, matabibu pamoja na mashabiki.

Katika pongezi zake Rais Infantino ameishukuru Yanga na TFF kwa kusadia kupeleka ujumbe chanya kwa jamii kuhusiana na soka