Pogba ajui kupika yai la kuchemsha

Wednesday April 19 2017

 

By London, England

Kiungo ghali wa Manchester United, Paul Pogba ameanza kuchukua darasa la upishi pamoja na somo la jinsi ya kuchemsha yai.

Kiungo huyo Mfaransa mwenye miaka 24, amekuwa akifundisha jinsi ya kupika na mpishi wake mkuu.

Mwanamke huyo Mtaliano amekuwa akimpikia chakulaPogba, pamoja na kumfundisha jinsi ya kuchemsha yai na kupika mayai na nyama ya kukaanga.

Pogba anayelipwa pauni 300,000 kwa wiki, pia anafundishwa kupika na vyakula vingine.

Mpishi huyo ndiye aliyekuwa akimpikia alipokuwa akicheza Juventus kabla ya msimu huu ujinga na Man United kwa uhamisho uliovunja rekodi ya dunia wa pauni 89 milioni.