Ng'ombe aitabiria mabaya Man United fainali Europa Ligi

Muktasari:

Utabiri huo ni habari mbaya kwa mashabiki wa Manchester United baada ya ng'ombe huyo mwenye jina la Sijtje kutabiri kikosi cha Jose Mourinho kitafunga katika mchezo wa fainali unaofanyika Stockholm.

London, England. Ng'ombe maarufu nchini Uholanzi ametabiri matokeo ya mechi ya fainali ya Europa Ligi kati ya Ajax na Manchester United itakayopigwa kesho, Jumatano.

Utabiri huo ni habari mbaya kwa mashabiki wa Manchester United baada ya ng'ombe huyo mwenye jina la Sijtje kutabiri kikosi cha Jose Mourinho kitafunga katika mchezo wa fainali unaofanyika Stockholm.

Miamba hiyo miwili Ulaya itakutana usiku wa kesho kusaka ubingwa wa mashindano hayo pamoja na kukakata tiketi ya kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao.

Kuelekea mchezo huo mwenye ng'ombe Sijtje, ambaye utabiri wake unatimia kwa asilimia85, aliamua kumwacha ng'ombe huyo kutabiri bingwa wa Europa Ligi.

Mmiliki huyo alichukua ndoo mbili na kuziweza nembo ya klabu hizo zikiwa sawa na ndani yake kuweka chakula.

Ng'ombe Sijtje aliyekuwa zizini alifunguliwa na kwenda kuchagua ndoo Ajax ikiwa ni ishara kuwa ndiyo watakaokuwa mabingwa.

Ng'ombe huyo alipatia utabiri wa uchaguzi wa Uholanzi wakati alipoekewa ndoo 11 zenye picha za wagombea. Pia alitabili matokeo ya ushindi wa Uholanzi dhidi ya Mexico wakati wa Kombe la Dunia 2014. .

Umaarufu wa ng'ombe Sijtje umekuwa ukiongezeka japokuwa bado hajafikia kiwano cha pweza Paul aliyetabiri kwa usahihi matokeo ya mechi 12 kati ya 14 za Kombe la Dunia 2010.