Mwanjali ana zali

Saturday January 7 2017

JEMBE la Simba, Method Mwanjali ameweka rekodi ya kuwa mchezaji wa kwanza kuchaguliwa kuwa mchezaji bora wa mechi (man of the match) mara mbili mfululizo katika michuano ya Kombe la Mapinduzi.

Mwanjali ambaye ni nahodha msaidizi Simba, alichaguliwa kuwa mchezaji bora wa mchezo wa Simba na KVZ ya visiwani hapa ambapo mchezo huo ulimalizika kwa Simba kushinda kwa bao 1-0.

Akionyesha kuwa hajabahatisha, Mwanjali alishinda tena tuzo hiyo wakati Simba ikitoka sare tasa na URA ya Uganda.