Mwamuzi Webb amaliza kifungo

Mwamuzi Rashid Farahan “Webb”

Muktasari:

Mwamuzi Webb aliyekuwa amefungiwa na ZFA,  alianza kibarua chake rasmi kwa kuchezesha mchezo nambari 189 ambao  Taifa ya Jang’ombe ilichapa Kilimani City kwa mabao 4-1.

Zanzibar. Mwamuzi Rashid Farahan “Webb” amemaliza kifungo chake cha miezi sita.

Mwamuzi Webb aliyekuwa amefungiwa na ZFA,  alianza kibarua chake rasmi kwa kuchezesha mchezo nambari 189 ambao  Taifa ya Jang’ombe ilichapa Kilimani City kwa mabao 4-1.

Katika mchezo huo Webb alionesha umahiri wake wa kupuliza kipyenga kiwanjani hapo kwa kutoa adhabu kama zinavyotokea, hakuna timu hata moja iliyolaumika baada ya mchezo huo kukamilika.

Mwamuzi Webb alifungiwa Novemba 15, 2016 na kamati tendaji ya ZFA taifa kutochezesha mpira wa miguu ndani ya Zanzibar kwa kipindi cha  miezi sita kufuatia kushindwa kuitafsiri sheria namba 10 ya soka inayohusiana na namna ya upatikanaji wa bao.

Mwamuzi huyo alifanya kosa hilo katika mchezo nambari 73 uliochezwa 11/11/2016 wakati Jang'ombe Boys ikichapa Miembeni 1-0 kwenye Uwanja wa Amaan.