Mwamuzi Man City na Man United huyu hapa

Muktasari:

Mechi hiyo inapewa nafasi ya kuwa yenye ushindani na kivutio kikubwa kwa timu hizo zinazosaka nafasi ya kumaliza kwenye nne bora msimu huu.

Mwamuzi Martin Atkinson amekabidhiwa kibarua cha kuchezesha mechi baina ya Manchester City na Manchester United inayofanyika kwenye Uwanja wa Etihad.

Mechi hiyo inapewa nafasi ya kuwa yenye ushindani na kivutio kikubwa kwa timu hizo zinazosaka nafasi ya kumaliza kwenye nne bora msimu huu.

Atkinson, tayari amechezesha mechi tatu za Manchester United na mbili za Manchester City msimu huu.

Ni mwamuzi ambaye mashabiki wa Man United walichukizwa naye baada ya kushindwa kumtoa kwa kadi nyekundu beki wa kati wa Chelsea David Luiz kwa madai ya kumchezea rafu  Marouane Fellaini, mchezo ambao Chelsea ilishinda 4-0  kwenye Uwanja wa  Stamford Bridge.

Hata hivyo, Atkinson amewahi kuchezesha mechi tatu baina ya majirani hao misimu iliyopita.

Msimu wa 2009/10, Manchester United ilishinda kwa bao la dakika za majeruhi la Michael Owen, mchezo ambao ulimalizika kwa matokeo ya 4-3 kwenye Uwanja wa  Old Trafford, ambako mkongwe Paul Scholes alifunga bao la kichwa.

Pia, mwamuzi huyo alichezesha mechi ambayo mshambuliaji  Robin Van Persie alifunga bao safi la adhabu ndogo, pia kwenye ushindi wa mabao  3-2 ugenini kwenye Uwanja wa Etihad Stadium msimu wa 2012.

Mwamuzi huyo alikosolewa na mkonge  Sir Alex Ferguson ambako aliambia kuwa laini kwenye mchezo baina ya Chelsea msimu wa 2011.