Mwamuzi Kikumbo kuchezesha Simba, Mbao

Muktasari:

Katika taarifa ya TFF iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano
Alfred Lucas ilisema kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya mashindano hayo shirikisho hilo limemtangaza Kikumbo kuchezesha fainali itakayofanyika Uwanja wa Jamhuri kesho kuanzia saa 10.00 jioni.

Dar es Salaam. Shirikisho la Soka Tanzania (TFF)limemteua mwamuzi Ahmed Kikumbo wa Dodoma kuchezesha mechi ya fainali ya mashindano ya Azam Sports Federation Cup kati ya Simba na Mbao kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri, Dodoma.

 Katika taarifa ya TFF iliyotolewa na Ofisa Habari na Mawasiliano
Alfred Lucas ilisema kwa mujibu wa Kanuni ya 13 ya mashindano hayo shirikisho hilo limemtangaza Kikumbo kuchezesha fainali itakayofanyika Uwanja wa Jamhuri kesho kuanzia saa 10.00 jioni.

Kikumbo atasaidiwa na Mohammed Mkono wa Tanga na Omary Juma wa Dodoma wakati mwamuzi wa akiba ni Florence Zablon pia wa Dodoma wakati Kamishna wa mchezo huo atakuwa Peter Temu wa Arusha.

TFF inazitakia timu zote, Simba, Mbao, Waamuzi pamoja na Kamishna na wanafamilia wa mpira wa miguu, mchezo mzuri wenye fanaka kwa kila upande.

Bingwa wa Kombe la ASFC atapewa kombe fedha shilingi milioni hamisini (50,000,000) pamoja na kufuzu kucheza mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika mwakani.