Msafara wa watu 40 kutua Mbio za Nyika Uganda

Muktasari:

Katibu Mkuu wa shirikisho la Riadha Nchi (RT) Wilhelm Gidabuday amesema kuwa kikosi hicho kilichokaa kambini kwa siku 24 kitakabidhiwa bendera mkoani hapa na Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo Nape Nnauye, kisha kuanza na safari.

Arusha. Kikosi cha wanariadha 28 pamoja na viongozi wa Shirikisho la Riadha Tanzania (RT) takribani 12, wanatarajia kwenda Uganda  keshokutwa kwenye mashindano ya Dunia ya Mbio za Nyika yatakayofanyika mwishoni mwa wiki katika Jiji la Kampala.

Katibu Mkuu wa shirikisho la Riadha Nchi (RT) Wilhelm Gidabuday amesema kuwa kikosi hicho kilichokaa kambini kwa siku 24 kitakabidhiwa bendera mkoani hapa na Waziri wa Habari, Utamaduni, sanaa na Michezo Nape Nnauye, kisha kuanza na safari.

“RT imeweka historia ya kipekee kwa kupeleka idadi ya wanariadha wote kama idadi ilivyotakiwa tangu mwaka 1991   na tayari tumepokea Pongezi kutoka shirikisho la riadha la Kenya baada ya kusikia Tanzania tumepeleka kikosi kizima kwenye mashindano hayo”