Mourinho aonya wanaomsakama Pobga

Friday May 19 2017

 

London, England. Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amewajia juu watu wanaohoji uhamisho wa Paul Pogba kwamba ulikuwa na kasoro msimu huu.

Pogba alihamia kwenye kikosi hicho cha Old Trafford akitokea Juventus Agosti mwaka jana  kwa uhamisho wa Pauni 89.3 milioni akivunja rekodi ilikuwa imewekwa na Gareth Bale ya Pauni 86 milioni kwenda Real Madrid mwaka 2013.

Kiungo huyo Mfaransa, hakufanya vyema awali alipojiunga na klabu hiyo ukilinganisha na thamani yake. Jambo hilo lilizusha mjadala huku mashabiki wakihoji kiwango chake uwanjani.

Pobga mwenye miaka 24 ameimarika mwishoni mwa msimu baada ya kuonyesha kiwango kizuri na kuleta mabadiliko kwenye safu ya ushambuliaji.

Pia kocha Jose Mourinho amesisitiza kwamba hana shaka na kiwango cha Pobga  hususani katika michezo aliyocheza kwenye Ligi ya Europa. Pia anatumaini  kwamba mchezaji mwingine ghari duniani atatokea kwenye kikosi hicho msimu ujao.

“Nafikiri tatizo lipo kwenye kulielezea jambo hilo, msimu ujao hakuna atakayesajiliwa ka fedha nyingi kiasi hicho lakini huenda likatokea kwa mwingine”

Akizugumzia kiwango cha Pobga, Mourinho alisema,  “Ameonyesha kiwango kizuri na amecheza mechi zote kwa umahiri mkubwa. Jambo la tofauti ni kwamba kila mtu anatarajia kiwango kinachoendana na uhamisho wake wa thamani kubwa.”