Mourinho anamuuza Herrera

Muktasari:

Gazeti la michezo maarufu la Hispania, Marca limedai kwamba kocha huyo wa Man United kwa siri kubwa aliwaambia Zlatan Ibrahimovic, Ander Herrera na zaidi David De Gea, kwamba hawezi kuwazuia kama wataamua kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.

HII imetokea huko Hispania. Ni hivi, inadaiwa kwamba Jose Mourinho amewaambia kwa siri mastaa wake watatu kwamba ruhusa kuondoka Manchester United.

Gazeti la michezo maarufu la Hispania, Marca limedai kwamba kocha huyo wa Man United kwa siri kubwa aliwaambia Zlatan Ibrahimovic, Ander Herrera na zaidi David De Gea, kwamba hawezi kuwazuia kama wataamua kuondoka Old Trafford mwishoni mwa msimu huu.
Taarifa zaidi imefichua kwamba ni suala la Mourinho tu kupanga bei ya mchezaji na kama kutakuwa na timu itakayopanda bei na kufikia dau wanalotaka basi watauzwa tu.
Marca liliendelea kuripoti kwamba Real Madrid wao wameweka wazi kumtaka De Gea, ambao wamemweka kwenye fungu la kwanza kabisa la wachezaji wanaowataka.
Lakini, Real Madrid bado hawafahamu ni kiasi gani cha pesa Man United itahitaji kwa kipa huyo chaguo la kwanza, licha ya kuwapo na taarifa huenda akapigwa bei kwa Pauni 51 milioni.
Marca limedai kwamba De Gea anafurahia maisha yake ya Manchester licha ya kwamba anafikiria mpango wa kutimkia Madrid. Real Madrid kwa upande wao wamepanga kuzungumza kwanza na kipa chaguo la kwanza Keylor Navas.