Mourinho amuonyesha jeuri De Gea

Muktasari:

  • Kipa huyo wa Manchester United amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Real Madrid kwa muda mrefu jambo lililomfanya Mourinho hawezi kumbakisha mchezaji yeyote asiyetaka kubaki.
  • Inaaminika kuwa Madrid imedhamiria kuvunja rekodi ya uhamisho ya makipa kwa kumchukua De Gea mwishoni mwa msimu huu na tayari Mourinho ameanza kuorodhesha makipa ambao wanaweza kurithi mikoba ya De Gea Old Trafford.

Kocha wa Manchester United, Jose Mourinho amemwambia kipa wake, David De Gea anaweza kuondoka mwisho wa msimu huu.
Kipa huyo wa Manchester United amekuwa akihusishwa na kutakiwa na Real Madrid kwa muda mrefu jambo lililomfanya Mourinho hawezi kumbakisha mchezaji yeyote asiyetaka kubaki.
Inaaminika kuwa Madrid imedhamiria kuvunja rekodi ya uhamisho ya makipa kwa kumchukua De Gea mwishoni mwa msimu huu na tayari Mourinho ameanza kuorodhesha makipa ambao wanaweza kurithi mikoba ya De Gea Old Trafford.
De Gea alikaribia kutua Santiago Bernabeu katika dirisha kubwa la majira ya joto mwaka 2015, lakini uhamisho huo ulivurugika katika saa 11 za mwisho kabla ya kufungwa kwa dirisha hilo na tangu hapo amekuwa akihus