Monaco yakataa dau la Liverpool kwa Mbappe

London, England. Pamoja na Liverpool kuonyesha nia ya kutaka kumsajili  Kylian Mbappe klabu yake ya Monaco imekataa dau la euro 75 milioni zilizotolewa na miamba hiyo ya England.

Makamu wa rais wa Monaco, Vadim Vasilyev amesema mshambuliaji huyo ataendelea kubaki Ufaransa.

Liverpool imeweka wazi nia yake ya kumtaka nyota huyo wa Ufaransa, lakini rais wa klabu ya Monaco, Dimitri Rybolovlev amesisitiza aina yoyote ya uhamisho inapaswa kusubili hadi mwakani.

MARCA inajua sababu ya Monaco kukata dau hilo kwa sababu wamepanga kuuza mchezaji huyo kwa gharama ya euro 100 milioni.

Mbappe amekuwa na msimu mzuri katika Ligi Kuu Ufaransa na Ligi ya Mabingwa jambo lililozivutia klabu nyingi za Ulaya.

"Tutafanya kila tuwezalo kuhakikisha nyota huyo anabaki hapa," Vasilyev aliimbia Canal.

"Tutafanya kila kitu, lakini itategemea na matakwa ya mchezaji mwenyewe."

Ikiwa imebaki mechi moja ya kufunga msimu huu, Mbappe amechangia mabao 40 yaliyofungwa na timu yake msimu huu katika mashindano yote, amefunga mabao 26, ametegeneza pasi 14 katika mechi 43.