Mkwasa awaacha Samatta, Ulimwengu Stars

Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu

Muktasari:

Kocha Mkuu wa Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 24 watakaingia kambini kwa ajili ya mechi Nigeria, Septemba 2, 2016.

Kocha Mkuu wa Taifa Stars’, Charles Boniface Mkwasa ameita wachezaji 24 watakaingia kambini kwa ajili ya mechi Nigeria, Septemba 2, 2016.

Taarifa iliyotolewa na TFF kupitia ofisa habari wake, Alfred Lucas ilibainisha kwamba timu hiyo itaingia kambini Jumatatu ijayo kwa kambi ya siku tano ambayo itavunjwa kabla ya wachezaji hao kuitwa tena kwa maandalizi ya mwisho kabla ya kuelekea Lagos kuikabili Nigeria au Super Eagles.

Safari hii Mkwasa amemuacha nahodha wa timu hiyo, Mbwana Samatta anayekipiga FC Genk ya Ubelgiji na Thomas Ulimwengu wa TP Mazembe ya DR Congo kutokana na majukumu ya klabu zao.

Hata hivyo nyota hao baadaye wataungana na wenzao Nigeria kwa kuwa mchezo huo upo kwenye kalenda ya Fifa.

Wachezaji aliowatangza jana ni makipa; Benny Kakolanya, Aishi Manula na Deogratius Munishi.

Mabeki ni Aggrey Moris, Mohammed Hussein 'Tshabalala, Kelvin Yondani, Oscar Joshua, Erasto Nyoni na Juma Abdul.

Viungo ni Himid Mao, Shiza Kichuya, Mohamed Ibrahim, Jonas Mkude, Mwinyi Kazimoto, Ibrahim Jeba, Juma Mahadhi, Farid Mussa na Hassan Kabunda

Washambuliaji ni Jamal Mnyate, Joseph Mahundi, Simon Msuva, Ibrahim Ajib, John Bocco na Jeremia Juma