Mkimchezesha Bukungu tu, mmekwisha

KATIKA mechi ya watani wa jadi leo Jumamosi Simba, inatazamwa kuwa na udhaifu wa beki wa kati ambaye ni mchezaji wa zamani wa TP Mazembe, Janvier Bokungu kama anavyoelezea nyota wa zamani wa Yanga, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’.

“Ni vyema wangemtumia beki Mganda, Juuko Murshid ambaye umri wake unamruhusu na ana kasi ambayo inaweza kuendana na mastraika waliopo Yanga, lakini kwa safu kama ya viungo Simba, wapo vizuri,” alisema.

“Zamani sisi hata kama hatujalipwa mshahara, ukiingia uwanjani unasahau yote unakuwa kama umekunywa maji ya bendera ya timu, hivyo tulikuwa tunajali kulinda heshima ili kuepusha watu kupata sababu,” alisema.

“Kwa sasa presha zimepungua kuhusu mechi hiyo na ndiyo maana mambo ya kuhama kambi siyo sana na wachezaji hawachukulii ukubwa wa mechi hiyo kwamba inakuwa na watu tofauti kama vile  mawakala hivyo inakuwa ni muda wao wa kujitangaza,” alisema.

Aliongeza kuwa: “Mechi ya Simba na Yanga, inaweza kumpandisha chati mchezaji ama kumbomoa kabisa na ndiyo maana inakuwa na presha, bahati mbaya nyota wa sasa hawatambui  jambo hilo,” alisema.