Mke, watoto wa Guardiola wanusurika shambulizi la Manchester

Muktasari:

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye TV3, familia ya kocha hiyo ilikuwepo wakati shambulio hilo likitokea.

Manchester, England. Taarifa zimetolewa leo kwamba mke na watoto wa Kocha wa Manchester City, Pep Guadiola imeelezwa walikuwa ni miongoni mwa watu waliokuwapo kwenye tamasha  kwenye Ukumbi wa Ariana Grand ambapo watu 22 waliuawa huku zaidi ya watu 50 wakijeruhiwa.

Kwa mujibu wa taarifa zilizopatikana kwenye TV3, familia ya kocha hiyo ilikuwepo wakati shambulio hilo likitokea.

Pia, inaelezwa baadhi ya wachezaji wa Manchester City ambao hawakutajwa majina yao walikuwepo na familia zao, lakini hawakuathiriwa na shambulizi hilo.

Mtandao rasmi wa wafuasi wa Guardiola “Pep Team Tweeter ulitoa pole kwa waathirika wa tukio hilo.

“Tumeshtushwa na shambulizi hilo  na tunashindwa kuamini kilichotoke. Salamu zetu za pole kwa ndugu jamaa na marafiki waliopata matatizo,” uliosomeka ujumbe huo.

Pia, mkutano wa klabu ya Manchester United na vyombo vya habari kuhusu mechi yao ya kesho umeahirishwa huku uongozi ukisisitiza kwamba mechi hiyo ipo palepale.