Messi wa Jang’ombe avunjiwa nyumba

Monday January 9 2017

Mshambuliaji wa Taifa ya Jang’ombe, Mohammed Said “Messi” amepata mtihani nyumbani kwao Malindi Mombasa nchini Kenya baada ya kuvunjiwa nyumba yao ili kupisha ujenzi wa barabara.

Messi amezungumza na Mwanaspoti: “Nilirudi nyumbani Malindi kwasababu nyumba yetu ilivunjwa kulikuwa kunatanuliwa barabara ya Malindi. Unajua nyumba yetu ipo karibu na barabara, kwahiyo zilivunjwa nyumba zote zilizokuwepo karibu na barabara, lakini sisi tunashukuru nyumba yetu haijavunjwa yote imepunguzwa kipande tu cha mbele.”

“Hapa unapopaona nilipata pia ajali kwenye Honda, huu mguu uliumia sana lakini kwasasa nashukuru Mungu naendelea vizuri maana kidonda kishakauka, sikuwa na raha maana karibu mwezi mzima niliokaa Kenya sikufanya mazoezi hata siku moja kwasababu ya hayo matatizo huku nyumba inavunjwa mara huku nikapata ajali, mitihani kwakweli.”