Mbappe amtoa udenda Conte

Muktasari:

Mbappe ameipeleka Monaco katika hatua ya nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa barani Ulaya na kuongeza thamani yake wakati huu Monaco wakidai kwamba, watakuwa tayari kumruhusu kwa timu ambayo itavunja rekodi ya uhamisho.

KOCHA wa Chelsea, Antonio Conte anataka kumuongeza kinda mahiri wa Monaco, Kylian Mbappe, 18 katika kikosi chake ingawa atalazimika kupambana na timu nyingi kubwa ambazo zinamtaka kinda huyo Mfaransa.