Mbappe aivuruga Real Madrid

Muktasari:

Mbappe amekuwa akitajwa kujiunga na miamba hao mabingwa wa Hispania huku naye akionyesha nia ya kuichezea klabu hiyo.

Hispania. Siku chache baada ya klabu ya England, Manchester City kuidaka saini ya mchezaji wa Monaco, Bernardo Silva jambo hilo limewashtua Real Madrid ambao wanamuwinda kinda Kylian Mbappe.

Mbappe amekuwa akitajwa kujiunga na miamba hao mabingwa wa Hispania huku naye akionyesha nia ya kuichezea klabu hiyo.

Kocha wa Real Madrid, Zinedine Zidane amekuwa akiumiza kichwa ili kuhakikisha mchezaji huyo nyota anatua Real Madrid kwa ajili ya kucheza msimu ujao.