Mashabiki kuilaki Simba jijini Dar es Salam leo

Muktasari:

  • Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, bao lililopatikana ndani ya dakika ngumu 120 katika mchezo ulipigwa jana Jumamosi makao makuu Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Dar es Salaam. Siku moja baada ya klabu ya Simba kutwaa ubingwa wa Kombe la Shirikisho kwa kuilaza Mbao FC ya Mwanza imeanza safari ya kurudi Dar es Salaam.

Simba iliibuka na ushindi wa mabao 2-1, bao lililopatikana ndani ya dakika ngumu 120 katika mchezo ulipigwa jana Jumamosi makao makuu Dodoma kwenye Uwanja wa Jamhuri.

Kwa matokeo hayo Simba imekata tiketi ya kupanda ndege na kuungana na watani zao Yanga. Simba watawakilisha Taifa kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho Afrika (CAF).