Mascherano abakia Nou Camp

Javier Mascherano

Muktasari:

KLABU ya Barcelona imetangaza kufikia makubaliano na Javier Mascherano juu ya mkataba mpya na ulioboreshwa wa miaka mitatu.

KLABU ya Barcelona imetangaza kufikia makubaliano na Javier Mascherano juu ya mkataba mpya na ulioboreshwa wa miaka mitatu. Nyota huyo wa kimataifa wa Argentina amekuwa akihusishwa na tetesi za kwenda Juventus ambao tayari wameshamsajili Dani Alves mapema kiangazi hiki.

Hata hivyo, mkurugenzi wa taasisi ya mahusiano Albert Soler amethibitisha kuwa Mascherano amekubali kubakia katika klabu hiyo aliyojiunga nayo mwaka 2010 akitokea Liverpool