Man City yaibomoa AS Monaco

Muktasari:

Kocha wa  Manchester City, Pep Guardiola amevamia klabu hiyo na kunasa saini ya  kiungo mshambuliaji, Bernard Silva kwa Pauni 60 milioni.

Siku chache baada ya AS Monaco kutikisa Ulaya kwa kikosi imara cha vijana machachari, klabu mbalimbali zimeanza kuimega klabu hiyo ya Ufaransa.

Kocha wa  Manchester City, Pep Guardiola amevamia klabu hiyo na kunasa saini ya  kiungo mshambuliaji, Bernard Silva kwa Pauni 60 milioni.

Silva alikuwa miongoni mwa makinda saba wa Monaco waliokuwa wakifuatiliwa kwa karibu na klabu tajiri Ulaya.

Nyota huyo wa  Ureno alitarajiwa kufanyiwa uchunguzi wa afya yake na juzi usiku aliwasili mjini Manchester.

Mbali ya Man City, Silva alikuwa akifuatiliwa pia na Manchester United. Aling'ara kwenye mechi mbalimbali za klabu hiyo ya Ufaransa iliyotolewa na Juventus ya Italia kwenye nusu fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Pia, Silva aliiwezesha  Monaco  kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu, Ligue 1 msimu huu akiwa na mabao manane kibindoni

Bernado mwenye miaka 22 aliyezaliwa Ureno, amekuwa mchezaji wa kwanza kutua Man City, anacheza zaidi kwa kutumia mguu wa kushoto.

Uhamisho wake umefanikishwa na uhusiano  mzuri baina ya klabu hizo mbili, Monaco na Man City .