Lwandamina, Mkata umeme wabaki

Monday March 20 2017

By GIFT MACHA, LUSAKA

KOCHA George Lwandamina ametumia fursa ya mapumziko ya Ligi Kuu Bara kuongeza muda wa kuendelea kubaki Zambia. Kocha huyo amekiri hawakuwa na bahati tu ndiyo maana walishindwa kuiondosha Zanaco katika raundi ya kwanza ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Lakini iliweka rekodi ya kutopoteza mchezo wowote katika mechi nne ilizocheza katika mashindano hayo kwa mwaka huu.

 Mabingwa hao wa kihistoria wa Ligi Kuu Bara walitoka sare na Zanaco katika mchezo wa kwanza kabla ya kupata sare tasa katika mchezo wa pili kitendo ambacho kiliwafanya wapinzani wao kusonga mbele kwa faida ya bao la ugenini.

Wakati huo huo, kocha Lwandamina pamoja na msaidizi wake Noel Mwandila na kiungo Justine Zulu wamebaki mjini hapa hadi siku ya Jumatano wakati timu ilirejea jijini Dar es Salaam jana Alfajiri.