Lwandamina: Hatukujiandaa

Thursday April 20 2017

 

By Doris Maliyaga

KOCHA Mzambia wa Yanga, George Lwandamina, ameyazungumzia mashindano ya CAF na namna walivyotolewa na MC Alger ya Algeria akisema: “Tulikuwa na mazingira magumu katika mchezo wetu wa marudiano (Yanga ililala 4-0).

“Kwanza mwamuzi alikuwa upande wao kwa kila kitu, hata hivyo sipendi kuzungumzia hilo.

“Pia, timu haikuwa na maandalizi mazuri, tumekwenda kwa kuchelewa na kuna mambo mengi tu ambayo tunatakiwa kuyafanyia kazi.

“Baada ya kuondolewa kwenye mashindano ya CAF nguvu zetu zote tunazihamishia kwenye ligi kuhakikisha tunachukua ubingwa. Hicho ndichi ninachowaahidi Wanayanga.

“Najua siyo kazi rahisi, lakini ni kupambana tutacheza mechi zote kama vita bila kujali udhaifu na ubora wa kikosi kwa sababu katika mapambano hiyo hakuna.”

Lwandamina amesisitiza kuwa kwa ubora wa kikosi chake, ni kuboresha mambo machache tu ili kuwa bingwa.