Luizio ahamasisha mashabiki wa Simba

Muktasari:

Luizio ameweka wazi hamu yao kuambulia taji hilo baada ya kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu na kuwapelekea mashabiki wao kukosa raha mtaani.

Luizio ahamasisha mashabiki wa Simba

Olipa Assa, Mwananchi

Dar es Salaam. Mshambuliaji Juma Luizio wa Simba, amewahamasisha mashabiki wa timu hiyo kufika kwa wingi kesho kwenye Uwanja wa Jamhuri Morogoro, kuwatia moyoa wakati wa mechi fainali ya Kombe la FA dhidi ya Mbao FC.

Luizio ameweka wazi hamu yao kuambulia taji hilo baada ya kuukosa ubingwa wa Ligi Kuu na kuwapelekea mashabiki wao kukosa raha mtaani.

"Naamini kwamba tutachukua ubingwa, ushirikiano wa mashabiki wetu na sisi kujituma naamini tutafuta machozi ya ligi kuu," anasema Luizio.