London Marathon wamwaga mamilioni

Muktasari:

Mashindano hayo yanayoshirikisha wakimbiaji wa mbio ndefu za maili 26.2, yatawahusisha wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali yatafanyika Jumapili hii jijini London.

Bingwa wa mashindano London Marathon atajinyakulia dola 100,000 msimu huu. hii.

Mashindano hayo yanayoshirikisha wakimbiaji wa mbio ndefu za maili 26.2, yatawahusisha wakimbiaji kutoka nchi mbalimbali yatafanyika Jumapili hii jijini London.

Katika mbio hizo ndefu wakimbiaji wanaotarajiwa kufukuza upepo kwa upande wa wanaume ni Kenenisa Bekele, Tesfaye Abera na Feyisa Lilesa. Pia wanawake ni Florence Kiplagat, Mary Keitany na Aselefech Mergia.

Waandaji wa mashindano hayo wameweka wazi zawadi kwa washindi wa kwanza wanaume na wanawake watajinyakulia kiasi cha Dola 55,000.

Washindi wa pili watazawadiwa Dola 30,000, wa tatu Dola 22,000 na mshindi wa nne ataondoka na Dola 15,000.

Pia mkimbiaji wa mbio ndefu ataondoka na kitita cha Dola 100,000  kwa wale watakaofanikiwa kumaliza kwa muda uliowekwa wa 2:05:00 na kwa wanawake 2:18:00.

Vilevile zawadi nyingine itatolewa kwa mshindi  wa mbio za 2:03:05 kwa wanaume  na wanawake mbio za 2:17:42.

Rekodi ya mbio hizo ndefu inashikiliwa na Mkenya, Eluid Kipchoge kwa wanaume na wanawake mshindi alikuwa Jemima Sumgong ambaye

hatatetea taji lake kutokana na kushindwa kukidhi vigezo wakati wa upimwaji wa dawa za kusisimua misuli, baada ya kuthibitika anatumia dawa hizo.