Liverpool yamtaka van Dijk

Muktasari:

Kocha wa Liverpool, Jurgen Klopp amepania kuzipiku klabu mbalimbali kubwa zinazomuwania beki huyo wa kimataifa wa Uholanzi ambaye alionyesha ukomavu mkubwa katika Ligi Kuu ya England msimu huu kabla ya kuumia.

Liverpool ipo tayari kuvunja rekodi yake ya uhamisho kwa kumchukua beki mahiri wa Southampton, Virgil van Dijk pindi dirisha la majira ya joto litakapofunguliwa mwishoni mwa msimu huu.