Soka

Lipuli waunda jeshi la ushindi

Share Bookmark Print Email
Email this article to a friend

Submit Cancel
Rating

 

By Charles Abel, Mwananchi ;cabel@mwananchi.co.tz  (email the author)
Email this article to a friend

Submit Cancel


Posted  Ijumaa,Mei19  2017  saa 11:49 AM

Dar es Salaam. Katika harakati za kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu msimu ujao, Lipuli FC ya Iringa imeteua kamati ya watu watano kusimamia maandalizi na usajili wao.

Mwenyekiti wa Lipuli, Abuu Majeki alisema kuwa kamati hiyo ya watu watano itaongozwa na Seif Kabange mwenyekiti atakayesaidiwa na mkurugenzi wa ufundi wa Lipuli, Delta Mshindo Msolla.

Wajumbe wengine ni kocha mkuu, Selemani Matola, meneja wa timu,  Mohamed Mrisho na Haruna Salehe.

"Timu imeanza rasmi zoezi la usajili na mwishoni mwa mwezi Juni tutaingia kambini huko Sumbawanga mkoani Rukwa, " alisema Majeki.

Lipuli imepanda Ligi Kuu msimu ujao baada ya kushika nafasi ya kwanza kwenye kundi A la ligi daraja la kwanza msimu huu.