Klopp aamua kufunguka

Kocha Jurgen Klopp

Muktasari:

KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp, amefunguka sababu ya kumrudisha nyumbani beki wake Mamadou Sakho badala ya kubaki naye kambini nchini Marekani.

KOCHA wa Liverpool Jurgen Klopp, amefunguka sababu ya kumrudisha nyumbani beki wake Mamadou Sakho badala ya kubaki naye kambini nchini Marekani.

Klopp alisema kwamba Sakho, ambaye hivi karibuni aliondolewa adhabu yake ya kufungiwa kutokana na tuhuma za matumizi ya madawa ya kusisimua misuli, alivunja sheria za klabu hiyo mara tatu na sasa ana hatihati ya kutemwa ikiwa kocha huyo atachukua maamuzi mazito zaidi.

“Ilikuwa ni almanusura achelewe ndege iliyobeba timu kutoka Liverpool kwenda San Francisco, alikosa mazoezi na timu, pia alichelewa kujumuika na wenzake kupata chakula,” alisema Klopp aliyetua Liverpool akitokea Borussia Dortmund.