Kimbunga kadi za kumwaga

WACHEZAJI wa Kijichi wakishangilia baada ya kuirarua timu ya Kimbunga mabao 3-1 katika mchezo wa Ligi Kuu Zanzibar Kanda ya Unguja.

KUNA timu nyingine zinawapa wakati mgumu kweli waamuzi kama ilivyofanya timu ya Kimbunga ambayo wachezaji wake watano walionyeshwa kadi za njano katika mchezo wao wa Ligi Kuu Zanzibar dhidi ya Kijichi uliofanyika wiki iliyopita na Kimbunga kulala kwa 3-1.

Ndiyo timu ya kwanza msimu huu kupigwa faini kwa kosa la kuoneshwa kadi hizo katika mchezo mmoja. Timu hiyo ya Mkoa wa Kaskazini Unguja imepigwa faini ya Sh50,000 kutokana na kosa hilo ambapo adhabu hiyo ni kwa mujibu wa kanuni za kuendeshea mashindano ya Ligi Kuu Zanzibar, kifungu cha 16(d).