Kaa mbali, Wawa anarudi sasa

Muktasari:

Wawa ambaye inadaiwa amebakisha mkataba wa miezi mitatu ndani ya kikosi hicho, alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti na baada ya uchunguzi tatizo alilokutwa nalo ni uchovu.

BAADA ya mchezo kati ya Azam FC na Ndanda FC ya Mtwara, klabu hiyo itaanza kupata huduma ya beki wao tegemeo, Muivory Coast, Serge Wawa aliyekuwa nje ya uwanja kwa kipindi kirefu.

Wawa ambaye inadaiwa amebakisha mkataba wa miezi mitatu ndani ya kikosi hicho, alikuwa akisumbuliwa na maumivu ya goti na baada ya uchunguzi tatizo alilokutwa nalo ni uchovu.

Kocha Mkuu wa Azam, Mhispania, Zeben Hernandez alisema kwamba alishindwa kumtumia Wawa katika mechi zilizopita kutokana na maumivu yaliyokuwa yakimsumbua.

“Kwa maumivu aliyokuwa nayo, Wawa asingeweza kusaidia timu na ndiyo maana tunasubiri apone kabisa na atakuwa vizuri baada ya muda mfupi,”alisema Hernandez.

Hata hivyo, Wawa alisema: “Kwa sasa namshukuru Mungu, hali yangu inaendelea vizuri nafikiri baada ya kutoka Mtwara, nitakuwa vizuri na kuisaidia timu yangu.”

“Mwanzo haitakuwa nzuri sana lakini anayejua anajua tu, kazi nzuri itafanyika. Wawa ni yule yule,” alisema Wawa