Juventus yaingia anga za Man United

Muktasari:

Kiungo huyo wa Bayern Munich amefanikiwa kucheza mechi sita tu msimu huu chini ya kocha Carlo Ancelotti na inavyoonekana anataka kuondoka sasa.

Turin, Italia. Juventus imeingia vitani na  Manchester United katika kuisaka saini ya chipukizi Renato Sanches.

Kiungo huyo wa Bayern Munich amefanikiwa kucheza mechi sita tu msimu huu chini ya kocha Carlo Ancelotti na inavyoonekana anataka kuondoka sasa.

Man United imesema inamtaka Sanches baada ya kumkosa msimu uliopita hivyo imerudi upya kwake.

Hata hivyo kwa mujibu wa Corriere dello Sport, Juventus limedai kuwa chipukizi huyo Mreno yuko mbioni kutua Turin ambako anaonekana atapewa nafasi ya kutamba zaidi Ulaya.

Mabingwa hao wa Italia wanaojiandaa na fainali ya Ligi ya Mabingwa kwa mara pili katika miaka mitatu na hivi karibuni wamekamilisha usajili wa winga wa Chelsea, Juan Cuadrado.