Herrera amtibulia De Gea

Friday May 19 2017

London, England. Mchezaji Ander Herrera amekuwa mchezaji bora wa mwaka wa klabu ya Manchester United msimu wa 2016/17 huku akizima ndoto za David De Gea.

Kipa huyo namba moja wa Manchester United alikuwa na matumaini makubwa ya kunyakua tuzo hiyo msimu huu hata hivyo hesabu zimevurugika.

Mchezaji huyo raia wa Hispania, amekuwa kwenye kiwango kizuri msimu huu jambo lililomshawishi kocha Jose Mourinho kumpa nafasi kwenye mechi za mashindano mbalimbali.

Herreara alinyakua tuzo hiyo jana Alhamisi akiwapiku wachezaji mahiri ambao walikuwa na matumaini ya kunyakua tuzo hiyo.

Mshindi huyo mpya wa msimu huu, alipata kura 242 huku akimuacha Zlatan Ibrahimovic akishika nafasi ya tatu, pamoja na Antonio Valencia akiwa nafasi ya pili.

Alisema, “Hii ni heshima kubwa kwangu lwa sababu niliona wachezaji niliokuwa nikishindana nao. Hapo ndio unaweza kubaini ni kwa namna gani jambo hili ni kubwa na muhimu.”