Hayatou ang'oka CAF

Issa Hayatou

Muktasari:

Katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali rais wa Shirikisho la Soka la Madagascar, Ahmed alipata kura 34 dhidi ya Hayatou aliyepata kura 20.

Addis Ababa, Ethiopia. Utawala wa miaka 29 wa Issa Hayatou umefikia mwisho baada ya kuangushwa na Ahmed Ahmed katika uchaguzi uliofanyika leo.
Katika uchaguzi huo uliokuwa na ushindani mkali rais wa Shirikisho la Soka la Madagascar, Ahmed alipata kura 34 dhidi ya Hayatou aliyepata kura 20.  
Hayatou aingia CAF na kuwa rais kwa mara ya kwanza 1988, tangu wakati huo hakuna kiongozi yeyote aliyefanikiwa kumtoa katika nafasi hiyo.
Mcameroon huyo alipata ushindani mkali kwa mara ya kwanza kutoka kwa  Armando Machado wa Angola (2000) na Ismail Bhamjee wa Botswana (2004), lakini wawili hao walishindwa kumnoa.