Fifa yampa tano Malinzi

Rais wa TFF, Jamal Malinzi.

Muktasari:

Rais wa Shirikisho la Kimataifa la Soka (Fifa), Gianni Infantino amemsifu Rais wa TFF, Jamal Malinzi kuwa ni miongoni mwa viongozi wa vyama vya soka duniani walioamua kuendesha soka kwa weledi kutokana na kuratibu mafunzo mbalimbali kwa makocha na waamuzi.

Salamu za Infantino zimetolewa na msimamizi mkuu wa kozi ya waamuzi nchini, Carlos Henrique kutoka Afrika Kusini akisema, “Infantino ana ripoti zote ya namna mpira wa miguu unavyoendeshwa duniani.

Anasifu Tanzania kwa  namna mnavyopiga hatua. Ana ripoti idadi ya makocha walivyokuwa wachache na sasa mna makocha wengine wako kwenye kozi.

“Mbali ya makocha, leo tuko nanyi waamuzi, ni hatua kubwa ambayo Rais Infantino amemsifu Rais wa TFF, Bwana Malinzi,” alisema Henrique.

Henrigue aliwataka waamuzi hao kujikita zaidi kusoma namna sheria 17 za soka zilivyoboreshwa kwa kuondoa zaidi ya maneno 1,000 ili kuja kusimamia vema soka.

Henrique katika kuendesha kozi hyo anashirikiana na Mark Mzengo kutoka Malawi, Felix Tangawarima wa Zimbabwe na Gladys Onyago kutoka Kenya.

Kozi ya waamuzi wa soka nchini ilianza jana Jumatatu kwa waamuzi wenye Beji za Fifa na waaamuzi waandamizi wanaotarajiwa kuveshwa beji hizo kwa majina yao kupendekezwa Fifa kama watapata matokeo mazuri kwenye kozi hiyo.