Farid Mussa kutimka zake Hispania

Straika chipukizi wa Azam, Farid Mussa. Picha ya Maktaba 

Muktasari:

April mwaka huu Farid alienda kufanya majaribio katika klabu ya Daraja la Pili ya Tenerife na kufaulu, kabla ya kurejea na kuonekana kama ndio basi tena, lakini uongozi wa Azam umethibitisha mchezaji huyo atatimka muda wowote.

STRAIKA chipukizi wa Azam na timu ya taifa, Taifa Stars, Farid Mussa wakati wowote anatarajia kutimka zake kwenda Hispani tayari kucheza soka la kulipwa.

April mwaka huu Farid alienda kufanya majaribio katika klabu ya Daraja la Pili ya Tenerife na kufaulu, kabla ya kurejea na kuonekana kama ndio basi tena, lakini uongozi wa Azam umethibitisha mchezaji huyo atatimka muda wowote.

Farid aliyekuzwa na kituo cha soka cha Azam Academy ni mmoja kati ya wachezaji wanaoonyesha watafika mbali kama wakiamua kukomaa kwa vike ana kipaji halisi cha soka pia anajitambua kwelikweli.