Familia ya Pogba yapamba Old Trafford

Friday February 17 2017

 

London, England. Mathias Pogba na mama yake Yeo walionekana uwanjani wakiwa wamevaa jezi nusu ya Manchester United na nusu St Etiennea.
Mama huyo alilazimika kuvaa hivyo akishangilia timu za watoto wake Paul na Florentin waliokuwa wakionyesha kazi uwanjani Old Trafford.

Mama Yeo Pogba aliyekuwa jukwaani akitazama mechi hiyo haikujulikana kama alishangilia wakati  Zlatan Ibrahimovic alipofunga mabao yake matatu.

Wakati alipoulizwa kama anashangilia timu gani kati ya  Manchester United na St Etienne, Mathias ambaye ni pacha wa Florentin alisema:  "siwezi kujigawa mwenyewe."

Mathias alikuwa amevalia jezi nusu ikiwa Man Unitedna nusu St Etienne na nyuma akiwa amebadika namba za ndugu zake na kuandika Pogba.