Fabregas kila pasi bao

Muktasari:

Wakati Chelsea ikishinda mabao 4-2 dhidi ya Southampton, kiungo huyo Mhispania alipiga pasi yake ya bao ya103 katika Ligi Kuu akilingana na mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard huku wakiachwa na Ryan Giggs aliyepiga pasi 162 za bao.

Kiungo Cesc Fabregas amepanda hadi nafasi ya pili katika orodha ya wachezaji waliotoa pasi nyingi za mabao katika Ligi Kuu England baada ya kumpigia krosi nzuri iliyofungwa na Diego Costa.
Wakati Chelsea ikishinda mabao 4-2 dhidi ya Southampton, kiungo huyo Mhispania alipiga pasi yake ya bao ya103 katika Ligi Kuu akilingana na mkongwe wa Chelsea, Frank Lampard huku wakiachwa na Ryan Giggs aliyepiga pasi 162 za bao.
Nyota huyo wa zamani wa Manchester United, Giggs aliyestaafu soka 2014 baada ya kutwaa mataji 13 ya Ligi Kuu huku akipiga pasi 162 za mabao katika maisha yake ya soka.