Fabregas humwambii kitu kwa Mourinho

Muktasari:

KIUNGO Cesc Fabregas amekiri kwamba hakuna kipindi alichofurahia sana kucheza soka katika maisha yake kama wakati akiwa chini ya kocha Jose Mourinho.

 LONDON, ENGLAND. KIUNGO Cesc Fabregas amekiri kwamba hakuna kipindi alichofurahia sana kucheza soka katika maisha yake kama wakati akiwa chini ya kocha Jose Mourinho.

Kiungo huyo wa Chelsea alisema kufanya kazi chini ya kocha huyo mpya wa Manchester United, Mourinho ni raha sana.

Mourinho, ndiye aliyemrudisha Fabregas kwenye Ligi Kuu England akitokea Barcelona na kutua Chelsea, lakini Desemba mwaka jana kocha huyo alipoteza kibarua chake Chelsea na sasa amejiunga na Man United.

Fabregas alisema: "Kufanya kazi na Mourinho ilikuwa poa sana.