Eto'o anukia kutua China

Muktasari:

  • Wakala wa Eto'o anataka klabu ya Yifang iwalipe karibu euro 4.5milioni kama mshahara, jambo ambalo linaoneka kuwa gumu kwa sasa, lakini kama mchezaji mwenyewe atakubali kupunguza dau hili basi atafanikisha uhamisho wake katika nchi ya sita kwenye maisha yake ya soka.

Madrid, Hispania. Mshambuliaji wa zamani wa Real Madrid na Barcelona, Samuel Eto'o anataka kufanya uhamisho mwingine kabla ya kustaafu soka.

Mshambuliaji huyo wa zamani wa Cameroon yuko mbioni kujiunga na klabu ya China ya Dalian Yifang itakayomlipa euros1.5 milioni kama watafikia makubaliano.

Klabu hiyo ya ligi daraja la pili China inafundishwa na Juan Ramon Lopez Caro ameonyesha nia ya kutaka kufanya kazi na Eto'o ambaye yuko tayari kutua Nyasha Mushekwi kama watafikia makubaliano.

Wakala wa Eto'o anataka klabu ya Yifang iwalipe karibu euro 4.5milioni kama mshahara, jambo ambalo linaoneka kuwa gumu kwa sasa, lakini kama mchezaji mwenyewe atakubali kupunguza dau hili basi atafanikisha uhamisho wake katika nchi ya sita kwenye maisha yake ya soka.

Kocha wa zamani wa Real Madrid, Caro anataka kuimalisha safu  ya ushambuliaji ya Dalian Yifang ili kuhakikisha timu hiyo inapanda daraja.