Enrique aaga Barcelona kwa taji la Copa del Rey

Muktasari:

Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Alaves.

Messi amemaliza msimu huu akifikisha jumla ya mabao 54 aliyofunga kwenye mashindano yote.

Hispania. Kocha wa Barcelona, Luis Enrique amehitimisha kibarua chake kwenye klabu hiyo baada ya kutwaa taji la Copa del Rey jana Jumamosi.

Barcelona iliibuka na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya timu ya Alaves.

Messi amemaliza msimu huu akifikisha jumla ya mabao 54 aliyofunga kwenye mashindano yote.

Kocha Enrique alishatangaza kuondoka klabuni hapo kabla ya msimu kuisha kutokana na presha ya mashabiki na uongozi wa timu hiyo baada ya kufanya vibaya kwenye michezo yake ya awali katika Ligi ya Mabingwa msimu huu.